Leviticus 8:7-9

7 aAkamvika Aroni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi. 8 bAkaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu
Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
kwenye hicho kifuko.
9 dKisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, yaani ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Copyright information for SwhNEN